Na Elinipa Lupembe
Hatimaye Mkoa wa Arusha umekuwa ni miongoni mwa mikoa nane nchini, kwa kufanikiwa kuingizwa kwenye program endelevu ya maji na usafi wa mazingira vijijini, program ya Lipa kutokana na Matokeo (P4R).
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa programu hiyo kwenye kikao kazi kilichowakutanisha viongozi na watalamu wa sekta mtambuka kutoka wilaya tano za mkao wa Arusha, Mkuu wa mkoa huo Mhe. John Mongela ameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia kwa kuona umuhimu wa kuuingiza mkoa wa Arusha kwenye programu hiyo muhimu kwa wananchi wa mkoa huo, mradi wenye lengo la kuongeza upatikanaji wa maji vijijini ifikapo 2025.
Amebainisha kuwa mkoa wa Arusha unakabiliwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wa maji, kutoaka na wananchi wa mkoa huo ni wakulima na wafugaji wanaotegemea maji kwa kiasi kikubwa huku asilimia 70 ya maeneo ya mkoa huo yanakabiliwa na ukame kwa kipindi kirefu cha mwaka, hivyo kukamilika kwa mradi huo unakwenda kutatua changamoto ya maji kwa wananchi waishio vijijini.
"Kwa niaba ya wananchi wa mkoa wa Arusha, tunamshukuru mheshimiwa Rais kwa jitihada kubwa za kutatua changamoto za wananchi waishio vijijini kwa kusogeza huduma muhimu ikiweomo maji, hivyo niwatake viongozi wa wananchi, wa siasa, wa dini kushirikiana na watalamu kiwaelimisha wananchi kutambua umuhimu wa mradi huu endelevu" Amesema Mhe. Mongella.
Fedha za program hii ni Lipa kutokana na Matokeo (PforR) mkoa umepewa kama mbegu, ambayo programu hii ikatekelezwa vizuri serikali italeta fedha nyingi zaidi za kutekeleza miradi ya maji na hatimaye uhaba wa maji mkoa wa Arusha kuwa historia, hivyo ni vema kila mtu kuhakikisha anashiriki kikamilifu katika utekelezaji wa mradi huu.
Mwenyekiti wa Bodi ya TARURA Tanzania Mhandisi Ruth Koya amewasisitiza watalamu kushirikiana na viongozi wa wananchi kuelezea vizuri manufaa ya mradi huu na kuongeza kuwa anaamini kukamilika kwa program hiyo kutasaidia kufikia adhma ya serikali ya kumtua mama ndoo kichwani kwa kuhakikisha maji yanapatikana karibu na makazi ya watu.
Naye Meneja wa TARURA mkoa wa Arusha Mhandisi Joseph Makaidi, amesema kuwa, programu hiyo itagharimu shilingi bilioni 4.8 na kutekeleza miradi 28 ya maji kwenye wilaya tano za mkoa wa Arusha, wilaya ya Arumeru, Monduli, Longodo Karatu na Ngorongoro, huku kila wilaya ikapata shilingi milioni 961.
Amesema kuwa, kukamilika kwa miradi hiyo kutaongeza asilimia 6 ya upatikanaji vijijini, huku miradi 24 inayoendelea kuongeza asilimia 6 na kufikia asilimia 85 za upatikanaji wa maji safi na salama vijijini ifikapo mwaka 2025 katika mkoa wa Arusha.
"Programu hii ina malengo ya kuwezesha upatikanaji wa maji vijijini, kuboresha huduma za usafi wa mazingira na usafi binafsi unatekelezwa na wizara ya maji na kusimamiwa na RUWASA, wizara ya Afya na wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia"Amefafanua Mhandisi Makaidi
Hata hivyo mkuu wa wilaya ya Karatu Mhe. Daudi Kolimba, licha ya kuishukuru serikali kwa programu hiyo inayokwemda kutatua changamoto ya ukosefu wa maji safi ja salama vijijini ameahidi kwenda kusimamia hatua zote za utekelzaji wa miradi hiyo ili ikamilike kwa wakati na viwanho vya ubora vilivyokubalika na kifikia lengo la serikali la kuwahudumia wananchi
Ikumbukwe kuwa utekelezaji wa mradi wa maji unakwenda sambamba na utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapindui ya mwaka ya kuhakikisha kufikia asilimia 85 ya uaptikanaji wa maji safi na salama vijiji na asilimia 95 mijini ifikapo mwaka 2025.
#KaziInaendelea
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.