Kamati ya ushauri ya Mkoa wa Arusha RCC, imepitisha shillingi bilioni 406.1 ikiwa ni rasimu bajeti ya mpango mapaoto na matumizi wa mkoa wa Arusha, kwa Mwaka ujao wa 2024 /2025.
Kamati hiyo imepitisha rasimu ya bajeti hiyo, wakati wa kikao cha kujadili utekelezaji wa shughuli za Mwaka wa fedha wa 2023/2024 kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha na Mwenyekiti wa kikao hicho, Mkuu wa Wilaya ya Karatu Dadi Kolimba, amewataka wajumbe wa kikao hicho kuwa mstari wa mbele na kuhakikisha wanasimamia vyema ukusanyaji Mapato katika halmashauri na Wilaya zao, ili kukabiliana na upotevu wa Mapato kutoka kwa watumishi wasio waamunifu .
Mbali na kupitisha bajeti hiyo wajumbe hao waliweza kujadili kuhusu ukusanyaji wa Mapato ambapo katika Mwaka 2023/2024, Mapato yanabainishwa kuongezeka kwa asilimia 7 ambapo halmashauri zilikusudia kukusanya shillingi bilioni 75 na katika Mwaka wa fedha 2024/2025 zimekusudia kuongeza na kukusanya shilingi bilioni 81 .
Aidha kaimu Mwenyekiti huyo amewataka wakuu wa Wilaya ikiwepo Wilaya ya Arusha Mjini kuhakikisha wanawachukulia hatua watumishi ambao si waaminifu, na wamekuwa wakifanya ujanja katika ukusanyaji wa Mapato .
Kwaupande wao wajumbe wa kikao hicho wameahidi kuweza kusimamia vizuri shughuli za ukusanyaji wa Mapato ili kutimiza azma ya Serikali ya kuwa na ukusanyaji wenye tija .
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.