Mwananchi wa kata ya Mateves halmashauri ya Arusha, wilaya ya Arumeru akiwasilisha kero yake kwa mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la soko la Kisongo Juni 04, 2024.
Mkutano huo umefanyika ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, aliposimama kuwasalimia wananchi wa kata hiyo, wakati wa ziara yake mkoani Arusha Juni 02, 2024 na kumtaka Mhe. Makonda kurudi kwenye kata hiyo rasmi, ili kusikiliza na kushughulikia kero za wananchi hao wa kata ya Mateves.
#ArushaNaUtalii
#kaziinaendelea ✍
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.