Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mheshimiwa Idd Hassan Kimanta amepokelewa rasmi leo katika ofisi yake na kuanza majukumu yake kama mkuu wa mkoa wa Arusha.
Akizungumza na watumishi wa umma, amewaomba ushirikiano katika kutekeleza majukumu yake ya kuleta maendeleo katika mkoa wa Arusha.
Kimanta amesema, uteuzi wake niwa wana Arusha nzima, hivyo kawataka kufanya kazi kwa upendo na kuaminiana.
Amewasisitiza watumishi wote wa mkoa wa Arusha kubadilika na kaucha kufanya kazi kwa mazoea kwani hizi ni zama tofauti zinazoitaji kuwatumikia wananchi kwa kasi kubwa.
Mheshimiwa Kimanta aliteuliwa mnamo Juni 19,2020 na mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli na kuapishwa Juni 22,2020 kama Mkuu wa Mkoa wa Arusha mpya.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.