Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Daktari John Pombe Magufuli amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mheshimiwa Idd Kimanta kusimamia migogoro yote iliyopo katika Mkoa wa Arusha.
Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza nae baada ya kumuapisha kama Mkuu wa mkoa mpya katika mkoa wa Arusha.
Mheshimiwa Magufuli, amewataka viongozi wote aliowateuwa mapema wiki hii kuhakikisha wanazingatia viapo walivyoapa katika kufanya kazi zao alizowatuma.
Nae, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mheshimiwa Selemani Jaffo,amewataka viongozi hao wapya kufanya kazi kwa ushirikiano baina ya wakubwa na wadogo na kuheshimiana.
Pia, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mheshimiwa Idd Kimanta amesema amelipokuwa jukumu hilo la kuwa Mkuu wa Mkoa kwa moyo wote na amesema anaona ni jukumu linalowahusu wana Arusha wote.
Kimanta amesema atashirikiana kwa ukaribu sana na viongozi wote wa Mkoa pamoja na wananchi kwa ujumla katika kuleta maendeleo ya mkoa mzima.
Viongozi walioapishwa leo hii ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mkuu wa wilaya ya Arusha, Mkuu wa wilaya ya Monduli,Mkuu wa wilaya ya Morogoro, Mkurugenzi wa Jiji la Arusha na Mkurugenzi wa Kaliua
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.