Na Elinipa Lupembe
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. John V.K. Mongella asubuhi ya leo amewasili kwenye ofisi za Mkuu wa wilaya Arusha tayari kwa ziara ya kikazi ya siku mbili ya kukagua utekelezaji wa shuguli za manedeleo kwenye Jiji la Arusha.
Katika ziara hiyo Mkuu huyo wa mkoa amemabatana na Kamati ya Usalama ya mkoa na atakagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo kisekta pamoja na kuzungumza na wananchi eneo la Soko la Kilombero na siku ya pili mkuatano wa Hazara eneo la Kwamrombo.
Hata hivyo mkuu wa wilaya ya Arusha, Mhe. Felician Mtahengerwa licha ya kumkaribisha mkuu huyo wa mkoa amemkaribisha katika Jiji la Arusha na kuweka wazi kuwa wako tayari kwa ukaguzi wa miradi na kupokea maelekezo atakayoyatoa
#ArushaFursaLukuki
#kaziinaendelea
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.