Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella amesema mpango wa m- mama uwafikie viongozi wa ngazi zote ili kuwajengea uwelewa wa pamoja.
Ameyasema hayo,alipokuwa akizindua mpango wa usafirishaji wa dharura wa Mama wajawazito, waliojifungua na watoto wachanga (m-mama) katika Mkoa wa Arusha.
Amesema,mpango huu utafanikiwa zaidi ikiwa utafika kwenye Kata, Vijiji Mitaa, na vitongoji kupitia kwa viongozi wa dini na kimila ili wao wakatoe elimu hiyo kwa wananchi ili iwe rahisi kuutumia.
Nae, Dororosa Duncan Mkurugenzi wa m- Mama Tanzania kutoka Vodacom foundation amesema mpango huo umeanzishwa baada ya kuona kuna changamoto ya vifo vya Mama na Mtoto katika jamii.
Amesema, wao wanashirikiana kwa karibu sana na Serikali ili kuhakikisha mpango huo unawafikia wananchi na kuleta manufaa zaidi.
Mratibu wa mpango wa m-mama Mkoa wa Arusha Getrude Anderson amesema Mkoa wa Arusha ulikuwa na vifo vya Mama na watoto 67 kwa mwaka 2019 hadi kufikia 2021 idadi ilikuwa vifo 50.
Mpango huu utasaidia kupunguza tabia ya uchekeweshwaji wa wagonjwa unaotokana na ukosefu wa usafiri hasa katika mazingira ya vijijini na hivyo kuendelea kushusha zaidi idadi ya vifo vya Mama na watoto.
Pia, mfumo huu utaenda kurasimisha utumiaji wa usafiri katika ngazi ya jamii kupatikana kwa urahisi.
Mpango wa usafirisha wa dharura kwa wajawazito waliojifungua na watoto ulinziduliwa rasmi Aprili 6,2022 na Rais Samia Suluhu hasani nakuanza kutekelezwa katika Mikoa ya Mwanza na Shinyanga.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.