Na Elinipa Lupembe.
Bohari Kuu ya Dawa (MSD) na Wadau wa Afya wanaohudumiwa na MSD, wametakiwa kushirikiana kutoa mawazo ili kuwa na mkakati wa pamoja, unakwenda kutatua changamoto za utaoaji na upatikanaji wa dawa na vifaa tiba, kwenye vituo vya kutolea huduma za afya, kutoka MSD, ili ziwafikie walengwa kwa wakati.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mhe. John V.K. Mongella, wakati akifungua Kikao Kazi, kilichowakutanisha watalamu wa MSD na Wadau wanaohudumiwa na MSD, Kanda ya Kilimanjaro, kinachofanyika kwenye Hoteli ya Masaai Land mkoani Arusha.
Mhe. Mongella amesema kuwa, licha ya changamoto zinazoikabili Bohari hiyo ya Dawa, ameweka wazi kuwa, yapo mabadiliko makubwa ya utendaji wa Bohari hiyo, unaendelea kurahisisha upatikanaji wa huduma ya dawa na vifaa tiba, kwenye vituo vya Afya vya mkoa wa Arusha.
Amesema kuwa kuna tofauti kubwa, ya uwepo wa dawa na vifaa tiba kwenye zahanati, vituo vya afya, hospitali za wilaya na hospitali za rufaa, jambo linalothibitisha utendaji kazi imara wa Serikali ya awamu ya sita, Wizara ya Afya na MSD, tofauti na vipindi vilivyotangulia hapo awali.
Hata hivyo Mhe. Mongella, amewataka wadau na watalamu hao, kupitia kikao kazi hicho kuja na suluhisho la kudumu la changamoto zilizosalia, katika kuhakikisha dawa na vifaa tiba vinapatikana kwa wakati na kuwahudumia wagonjwa, huku wakitambua kuwa, Afya ni nguzo kubwa ya maendeleo kwa mwananchi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
"Serikali ya Mama Samia, imefanya kazi kubwa sana katika sekta ya Afya, na inatambua na kuthamini kazi kubwa inayofanywa na MSD kwa sasa, tofauti na tulikotoka, kikao kazi hiki kitoke na mipango ya utatuzi wa changamoto na sio kuziorodhesha, kazi kubwa mliyonayo ni kutoka na mbinu za ufumbuzi zijikita kwenye suluhisho la changamoto, ili kufikia malengo ya serikali" Amesema Mhe. Mongella.
Licha ya kupongeza kazi kubwa na nzuri inayofanywa na MSD, amewataka watalamu hao kutambua kuwa, malalamiko yanayoelekezwa kwenye sekta ya Afya, yanabainisha wazi, unyeti wa huduma wanayoitoa, kwamba inagusa moja kwa moja mahitaji ya jamii kwa mtu moja moja hivyo ni vema kuwa na mkakati thabiti wa kuondoa malalamiko hayo.
Aidha, Mhe. Mongella, amewataka MSD, kuimarisha mifumo ya TEHAMA katika utoaji wa Dawa na Vifaa tiba ili kuimarisha mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya nchini pamoja na kufanya tathmin na kuhakikisha wanafanya kazi kwa pamoja ili kila upande uweze kutimiza wajibu wa kumhudumia mwananchi.
Awali Meneja wa Bohari ya Dawa, Kanda ya Kilimanjaro
Kikao kazi hicho cha mwaka, kinawakutanisha MSD na Wadau wanaohudumiwa na MSD wa mikoa ya kanda ya Kaskazini ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara.
#ArushaFursaLukuki
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.