Na Elinipa Lupembe
Mtumishi wa Mungu Mtume Boniface Godwin Mwamposa amefika kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa Mhe. John V.K. Mongella leo 27.10.2023.
Licha ya Kusaini kitabu cha wageni, Mtume Mwamposa amemueleza mkuu wa mkoa wa Arusha kuwa, yuko mkoani hapo kwa ajili ya huduma ya Mkutano neno la Mungu kwa muda wa siku tatu, unaokwenda kwa jina la 'Washa Taa, unaofanyika eneo la Kisongo karibu na uwanja wa Ndege Arusha.
Mtume Mwamposa ameshukuru kuwepo mkoani Arusha na zaidi kushukuru kwa kukutana na Mkuu wa mkoa huyo, ambaye amekiri kuwa amefanyika baraka katika mkoa huo kutokana na Mamlaka aliyopewa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
"Sisi watumishi wa Mungu tunaamini Mamlaka zote zinatoka kwa Mungu, hivyo Mkuu wa mkoa Mhe. Mongella ni Mamlaka ya Mungu, ninakutakia Baraka wewe na wananchi wote wa mkoa wa Arusha, huduma ya Washa Taa inakwenda kumulika mkoa wa Arusha na wananchi wake wote" Ameomba Mtume
Hata hivyo Mhe, Mongella amemkaribisha Mtume Mwamposa kwa kumuhakikishia hali ya amani, utulivu na usalama, na kuongeza kuwa Serikali inatambua na kuthamini kazi kubwa inayofanywa na watumishi wa Mungu, hususani huduma ya 'Rise & Shine' inayosimamiwa na Mtume Mwambosa.
Amefafanua kuwa, Mheshimwa Rais amesisitiza kutoa ushirikiano kwa watumishi Mungu wanaotoa huduma za Kiroho, kwa kuwa huduma hizo licha ya kuwaponya wananchi kiroho inahamasisha na kuchochea maendeleo ya nchi kwa kusisitiza kila mtu kufanya kazi kama yalivyo maandiko matakatifu.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.