Kiongozi wa Kanisa la Arise and shine (Inuka uangaze), lenye makao yake Makuu Jijini Dar Esamefika, Mtume Boniface MwamLaki amewasili mkoani Arusha na kutembelea kwenye viwanja vya Lakilaki - Kisongo eneo yatakapofanyika mashindano ya SAMIA MOTOCROSS CHAMPIONSHIP na kuungana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda na kukagua njia za mashindano hayo mapema leo Julai 12, 2023.
Mtume Mwamposa ameshiriki sala maalum ya kuombeachampionshiphayo ya pikipiki pamoja na kumuombea kheri, hekima na ubunifu wa ziada Mkuu wa Mkoa huyo Mhe. Makonda pamoja na kuwatia moyo washiriki wa mashindano kuwa vipawa walivyo navyo ni vya thamani kutoka kwa Mungu, hivyo mashindano hayo yakawe baraka ili vipawa hivyo vikazae baraka.
Mtume Mwamposa ambaye yuko Arusha akiambatana na Wachungaji wengine wa kanisa hilo, amempongeza pia Mhe. Makonda kwa kipawa na Neema kubwa aliyonayo katika dhamira yake njema ya kustawisha maisha na ndoto za vijana wengi wa kitanzania, akimtaka kuendelea kushughulika na ustawi wa wananchi anaowaongoza.
"Wote mnakubaliana kwa Rais wetu kumteua Mhe. Paul Makonda kwamba Mungu alimuongoza kumleta Arusha. Mhe. Makonda tumefahamiana tangu akiwa chuoni na kazi hizi anazozifanya sasa sio kwa bahati, Mungu amempa hicho kipawa na Mungu amempa hiyo Neema, Mungu amempa ufahamu wa kufanya mambo makubwa tangu nimemfahamu", Ameongeza Mtume Mwamposa.
Mashindano ya Samia Motocross Championship yanafanyika Jumapili hii Julai 14, 2024 kwenye viwanja vya Lakilaki Kisongo.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.