Mtume Boniface Mwamposa wa Kanisa la Arise and shine (Inuka Uangaze),Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii NSSF pamoja na Mfanyabiashara na Mmiliki wa Kampuni ya Utalii ya Leopard Tour wametoa Pikipiki 60 kwa Jeshi la Polisi Mkoani Arusha ili kuendeleza jitihada za Kuimarisha Ulinzi na usalama na kuchochea ukuaji wa Utalii Mkoani Arusha.
Pikipiki hizo 20 kutoka kwa Mtume Mwamposa, 20 kutoka NSSF na 20 kutoka kwa Leopard Tour zimetolewa na kukabidhiwa leo kwa Mkuu wa Mkoa Mhe. Paul Christian Makonda, ambapo Mtume Boniface Mwamposa ameahidi kuendelea kujitoa kwa Wananchi wa mkoa wa Arusha kama sehemu ya kuchangia kwenye maendeleo ya Mkoa huo wa Kaskazini mwa Tanzania ulio kitovu cha Utalii wa Tanzania.
Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha na Kamanda wa Polisi mkoani Arusha Justine Masejo wameshukuru kwa msaada huo, Huku RPC Masejo akiahidi kuzitumia kikamilifu pikipiki hizo katika kuhakikisha ulinzi na usalama wa Mkoa wa Arusha unaimarika na kuwa kivutio kwa wenyeji na wageni wa Mkoa wa Arusha wanaofika kwaajili ya shughuli mbalimbali za mikutano, biashara na Utalii.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.