Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.John Mongella leo ameupokea Mwenge Maalum wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Makongoro Nyerere katika Kijiji cha Kansay Wilaya ya Karatu.
Mwenge Maalum wa Uhuru ukiwa Mkoani Arusha utakagua, kufungua, kuweka Jiwe la Msingi na kutembelea miradi 53 yenye thamani ya sh. bilioni 5.8 kwa umbali wa Kilometa 959.35
Mwenge utazunguka katika Wilaya zote 6 za Mkoa wa Arusha, ambapo umeanza na Wilaya ya Karatu, Monduli, Arusha Jiji, Arumeru, Longido na mwisho Wilaya ya Ngorongoro na utakabiziwa Mkoa wa Mara mnamo Juni 22, 2021.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.