Mwili wa Waziri Mkuu Mstaafu, Hayati Edward Ngoyai Lowassa umewasili mkoani Arusha kwa ndege ya shirika la Ndege Tanzania na Kupokelewa na mamia ya wakazi wa mikoa ya Kanda ya Kaskazini wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. John V.K Mongella leo Februari 14, 2024.
Hayati Edward Ngoyai Lowassa, amefariki dunia Februari 10, 2024, anatarajiwa kuzikwa nyumbani kwake Ngarashi mjini Monduli Februari 17, 2024
Awali Rais wa Jamhuri ya Muungamo wa Tanzania Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuongoza watanzania katika mazishi ya hayati Edward Lowassa.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.