Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Doto Mashaka Biteko leo Oktoba 09, 2024 amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda kwa ubunifu wake katika Uongozi, suala ambalo limechangia kuitangaza Arusha kimataifa na kuvutia wageni na mikutano mingi zaidi kwenye Mkoa huo wa Kaskazini mwa Tanzania.
Akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Wataalamu wa Mionzi kutoka barani Afrika kwenye Kituo cha kimataifa cha mikutano cha AICC Jijini Arusha, Naibu Waziri Mkuu amesifu pia mapokezi mazuri wanayoyapata wageni na Viongozi mbalimbali wanapokuja Arusha kwaajili ya shughuli mbalimbali na kusema ugeni huo umesaidia pakubwa kusisimua uchumi wa Mkoa wa Arusha.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.