Na Elinipa Lupembe.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko (MB) ametoa Maelekezo 10 kwa Maafisa Mipango Nchini, Wakati akifungua Kongamano la Wanamipango 2023, liliofanyika mkoani Arusha, kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha ( AICC).
1. Washiriki wa wiki ya Mipango tumieni maarifa mtakayopata kwenye mafunzo kufanya maboresho ya utendaji kazi wenu.
2. Pelekeni dhana ya ushirikishwaji kwa wananchi na wadau wote katika Mipango yote ya maendeleo inayowahusu wananchi.
3. Mipango yote inayoandaliwa izingatie ushirikishwaji wa wadau wengine, wanaohusika katika mipango na miradi inayotekelezwa ili kujenga uelewa wa pamoja na hatimaye kuondoa upishani wakati wa utekelezaji
4. Wakurugenzi wa Mipango, zingatieni utamaduni wa kuwa na mawazo ya pamoja, katika kupanga Mipango ya Serikali na nchi kwa jumla, ili kuleta mipango imara itakayosaidia taifa letu, katika uchumi unaohitajika.
5. Wanamipango wamepewa jukumu la kusimamimia miradi, ufuatilia pamoja na tathmini, wazingatie utaratibu wa kutoa taarifa za utekelezaji wa program na miradi ya maendeleo, inayotekelezwa kwenye maeneo yao.
6. Shughuli za tathmini na ufuatiliaji zipewe kipaumbele kwa kutengewa rasilimali za kutosha, Idara ya Mipango zisiwepo tu kwa hisani ya Mkuu wa Taasisi, bali kwa maendeleo ya Taasisi, wananchi na Taifa
7. Maafisa Mipango wabadilike na kufanya tathmini ya miradi ya maendeleo na program zote, zitakazoelekezwa katika maeneo yenu, ikiwa ni pamoja na kwenye Mamlaka za Mikoa, serikali za mitaa na Taasisi za Umma.
8. Maandalizi ya Dira ya maendeleo ya mwaka 2050, yameanza utekelezaji wake, na kutokana umuhimu wa Dira ya Taifa letu, Wanamipango na wadau wengine wote ni muhimu kila mmoja kushiriki kikamilifu, katika hatua zote za maandalizi kama inavyohitajika.
9. Tume ya Mipango iweke Utaratibu wa kushiriki katika makundi mbalimbali ya wananchi na wadau wengine ili wachangie maoni ya Dira katika maandalizi yake.
10. Wananchi wote washiriki katika kutoa maoni yao kuhusu Tanzania wanayoitaka miaka 25 ijayo.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.