• Complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Arusha Regional

The United Republic of Tanzania President Office Regional Administration and Local Government Arusha Regional

  • Home
  • About Us
    • History
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa mikoa waliopita-Arusha
    • Dira na dhima
    • The basics
    • Strategies
  • Administration
    • Structure
    • Departments
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Units
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • District
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Councils
    • Arusha CC
    • Arusha DC
    • Meru DC
    • Monduli DC
    • Karatu DC
    • Longido DC
    • Ngorongoro DC
  • Investment Opportunities
    • Tourism
    • Livestock
    • Agricultre
    • Industrial
  • Our Service
    • Health
    • Education
    • Water
    • Land
    • Tourism
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

VIONGOZI KUTOKA NCHI 7 ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI WAMEZINDUA BARABARA YA BYPASS-ARUSHA

Posted on: July 22nd, 2022


Rais Samia Suluhu Hassan amewaasa wananchi kulinda na kutunza  miundombinu inayojengwa kwa gharama kubwa ili iendelee kudumu na kuimarisha uchumi wa nchi za Afrika Mashariki ( EAC).

Aidha, amemhakikishia Rais Uhuru Kenyatta ambaye anamaliza muda wake wa uongozi hivi karibuni mipango yote waliojiwekea ikiwemo ujenzi na miundo mbinu ya barabara ataikamilisha kama walivyokubaliana kwenye vikao vyao.

Akizungumza hayo jijini Arusha wakati alipokuwa kwenye hafla ya ufunguzi wa barabara ya Arusha Bypass ya Km.42.4 yenye thamani ya Dola milioni 217 kutoka Benki ya Maendelo ya Afrika (AfDB) ambayo kwa  Tanzania imetumika Dola milioni 212 na Kenya milioni 105.

Alisema ameona licha ya jitihada za ujenzi wa miundombinu unaofanywa na serikali pamoja na nchi za EAC kumezuka tabia ya uharibifu wa miundo mbinu hiyo ikiwemo kuiba vyuma vya madaraja na utupaji wa taka kwenye madaraja.

"Niwaombe sana watanzania tuheshimu na kufuata taratibu zilizowekwa katika utunzaji wa barabara kwa sababu imezuka tabia ya  baadhi ya watu kuharibu miundo ya barabara pamoja na  kutengeneza magari barabarani na kumwaga mafuta machafu yanayosababisha kuharibu miundombinu ya  barabara iliyotengenezwa kwa fedha nyingi,"alisema.

Samia,alisema serikali ya Tanzania  inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya miundombinu ya Reli,barabara,usafiri wa anga na majini ili kuunganisha nchi za EAC.

Aidha aliwataka wananchi ambao miundombinu hiyo inatekelezeka katika maeneo yao kutumia fursa za ujenzi wa miundombinu hiyo  kujikwamua kiuchumi.

Rais Uhuru Kenyatta aliwataka wananchi kuendelea kuunga mkono viongozi wa nchi za EAC ili waendelee kuashirikiana kwa pamoja katika kuleta maendeleo kupitia umoja wao ambao utasababisha waheshimike na mataifa makubwa Dunia.

" Ni ishara kubwa  kuwa viongozi tukiungwa mkono tukashirikiana kwa pamoja hakuna changamoto itakayotushinda tutafanya maendeleo makubwa kupitia umoja wetu na kuheshimika na mataifa Makubwa Duniani,"alisema .

Kuhusu barabara hiyo Rais Kenyatta alisema itasaidia kuunganisha nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na kurahisisha usafiri wa bidhaa mbalimbali za mboga mboga na mazao ya biashara.

"Huu ni utajiri mkubwa wa fursa katika kukuza uchumi wa nchi wanachama hasa kwa wakulima wa Tanzania ambao gharama za kusafirisha mazao yao zitapungua kutokana na uwepo wa barabara hii,"alisema

Kenyatta alitumia fursa hiyo kumpomgeza Rais Samia ambaye alipokea  nchi katika kipindi cha majonzi na watu wengi walikua na hofu,lakini amekuwaa hodari na mchapakazi na Taifa linasonga mbele.

"Kuna msemo wa Kiswahili unasema, usimuone Simba amenyeshewa ukadhani ni Paka dada yangu Rais Samia alipokea nchi katika kipindi cha majonzi na wengi walikuwa na hofu,lakini amekuwa ujasiri na mchapa kazi,"alisema.

Naye Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,Dk.Peter Mathuki alisema Afrika inahitaji kufikia mtengamano katika kukuza uchumi kwa kuwa na Miundombinu imara na viwanda vya kutengeneza bidhaa zitakazokuza  uchumi.

"Barabara hii ni muhimu katika kuimarisha biashara kwa nchi wanachama wa EAC", alisema.

Alisema moja ya mipango ya EAC ni kuimarisha uchumi ambapo wameweka vipaumbele vitano vilivyopewa msukumo mkubwa.

Alivitaja vipaumbele hivyo kuwa ni usafiri wa anga,Reli,Tehama,bandari na usafiri wa majini.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof.Makame Mbarawa alisema barabara hiyo itapunguza urefu wa safari kutoka Tanzania hadi Mombasa nchini Kenya.

Alisema barabara hiyo itafungua fursa  nyingi za kiuchumi na kijamii kwa nchi wanachama hasa Tanzania.

Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) nchini Tanzania Patricia Laverley  benki hiyo imetoa fedha hizo kwa ajili ya kusaidia  maendeleo na kuimarisha uchumi kwa nchi za EAC.

Aliahidi kuendelea kushirikiana  na nchi za EAC katika kutekeleza miradi ya maendeleo kwa sababu wamekiri malengo ya kuanzishwa kwa benki hiyo.

Announcements

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • View All

Latest News

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • View All

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
More Videos

Quick Links

  • Guildlines Towards the use of ICT In Government
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Public Servant Portal
  • Takwimu
  • TANAPA

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap
    • FAQ

Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.