Halmashauri za Mkoa wa Arusha zimetakiwa kuhakikisha zinabuni njia tofauti za ukusanyaji wa mapato kwa kutafuta vyanzo mbalimbali.
Maagizo hayo yametolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella alipofanya ziara ya kujitambulisha na kukagua miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Monduli na Jiji la Arusha.
"Ongezeni vyanzo vya mapato,vilivyopo havitoshi kabisa, kwani ni miradi mingi inatakiwa kuanzishwa hivyo vyanzo vilivyopo havita tosha kulingana na hali ya uchumi wa sasa".
Amesema Mkoa wa Arusha hauwezi kuendelea kutegemea mapato ya Utalii tu kwani sekta hiyo kwa sasa mapato yake ni kidogo, hivyo vinaitajika vyanzo vingine vyakuinua mapato ya Mkoa.
Aidha, amesisitiza katika usimamizi mzuri wa fedha zote zitakazokusanywa kutoka kwenye mapato hayo na hata za nje, ili ziweze kutumika katika shughuli husika.
Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe. Edward Balele, amesema Wilaya yake itasimamia kwa ukamilifu ukusanyaji wa mapato.
Nae, Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Kenan Kihongosi amesema Wilaya yake inaenda kufanyia kazi maelekezo yote waliyopokea na Mkuu wa Mkoa kwani Wilaya yake ndio jicho la Mkoa mzima.
RC Mongella amefanya ziara ya kikazi katika Wilaya ya Monduli na Jiji la Arusha ambapo amekagua miradi ya Afya, shule, Barabara, mshamba ya mbogamboga na Maji.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.