Maafisa maendeleo ya jamii wa Halmashauri ya Arusha wametakiwa kushirikiana na maafisa maendeleo ya kata zao katika kuhakikisha mpango kazi wa kupinga unyanyasaji dhidi ya wanawake na watoto katika halmashauri hiyo unatekelezeka.
Maelekezo hayo yametolewa na Mchumi Mkuu wa Mkoa bwana Moses Mabula alipokuwa akifunga kikao cha siku 3 cha tathimini ya utekelezaji wa mpango wa Taifa wa kupinga unyanyasaji dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA).
Aidha, amewaomba wadau wakiwemo shirika la SOS kuendelea kutoa ushirikiano hasa katika maeneo ambayo Serikali itaitaji ushirikiano na pia maafisa maendeleo ya Jamii kata washirikishe Jamii zenye uwezo katika kuchangia shughuli za maendeleo.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.