Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Richard Kwitega,amewataka waandishi wa Habari wakawe mabalozi wazuri wa kutangaza miradi mbalimbali iliyotekelezwa na mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF).
Ameyasema hayo alipokuwa akifungua mafunzo ya siku mbili kwa waandishi wa habari wa kanda ya Kaskazini, yaliyoandaliwa na TASAF jijini Arusha.
TASAF mpaka sasa imeshatimiza miaka 20 tangu kuanzishwa kwake na miradi mbalimbali imeanzishwa chini ya program hii kama vile;miradi ya maji, afya,na shule.
Pia,TASAF imeweza kugusa maisha ya watu kwa kuanzisha miradi ya ufugaji.
Waandishi wa Habari wana nafasi nzuri ya kuisahihisha jamii juu ya taarifa mbalimbali za miradi iliyotekelezwa na TASAF awamu zote.
Mafunzo hayo kwa waandishi wa Habari yamejumuisha mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Tanga katika kutoa dira ya mpango mpya wa TASAF awamu ya 3.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.