Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda amemshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na kuweka wazi kuwa, mhe Rais amewapa heshima kubwa wananchi wa mkoa wa Arusha.
Mhe. Makonda amesema hayo , wakati akifungua hafla ya Usiku wa Nyama Choma na Maadhimisho ya miaka 25 ya Jumuiya ya Nchi za Afrika Mashariki, mkesha uliofanyika Jijini Arusha usiku wa Novemba 28 kuamkia Novemba 29, 2024
"Ninamshukuru Mhe. Rais kwa kuona umuhimu wa nchi zoye nane zote za Afrika Mashariki kushiriki mkesha huu maalum kwa ajili ya kuadhimisha miaka 25 ya Jumuia ya nchi za Afrika Mashariki, mkesha uliokwenda sambamba na Usiku wa nyama choma, Popote nitakapokuwa nitahakikisha heshima yake inalindwa" . Amesema Mhe. Makonda Makonda Rc Paul
Aidha, amemshukuru kwakukubali mkoa wa Arusha kuwa kitovu cha Utalii hukua akiahidi kujadili maendeleo ya sekta ya utalii kwa kujadiliana na wadau wakubwa wa Utalii mkoani Arusha.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.