Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mheshimiwa Idd Hassan Kimanta, amesema atahakikisha anakuza Sanaa kwa kasi kubwa katika Mkoa huo, hasa mchezo wa Mpira wa Miguu, Mpira wa Pete,Riadha,Mziki na mingine mingi.
Ameyasema hayo alipokuwa akizindua bendi mpya ya muziki wa dansi ali maarufu kama Wisdom Musika katika Ukumbi wa Orlando jijini Arusha.
Amesema ,Sanaa ni nzuri kwani inatengeneza ajira kwa vijana na kuongeza nguvu ya kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
Amewataka wana sanaa wapendane na kuacha chuki ili Sanaa iweze kukua katika nchi na hata nchi za nje,kwani kukuza Sanaa ni moja ya mipango ya serikali katika kuleta maendeleo kwa wananchi.
Kimanta amewaomba wananchi wa Arusha kumuunga Mkono katika shughuli mbalimbali za kuleta maendeleo alizozipanga kuzifanya katika Mkoa kwa kufanya kazi kwa bidii,hivyo kuweza kumuunga Mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuri ambae anasisitiza kufanya kazi kwa bidii.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.