Kongamano la Uwekezaji katika Sekta ya Utalii nchini, linafanyia Aprili 30, 2024 kwenye Ukumbi wa Mkutano Hoteli ya Gran Melia.
Mgeni Rasmi katika Kongamano hilo ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb)
Katika Kongamano hilo Wizara ya Maliasili na Utalii chini ya Waziri Mhe. Angela Kairuki (Mb) @angellah_kairuki, watawasilisha mada za fursa za Uwekezaji Mkoa wa Arusha kwa kuzingatia Matokeo ya Program ya Tanzania The Royal Tour
Aidha, Kongamamo hilo limenadaliwa na Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Kauli Mbiu: Uwekezaji Katika Utalii Endelevu, Uchangamkiaji wa fursa za Uwekezaji baada ya Program ya Tanzania 'The Royal Tour'.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.