Kwa kipindi cha mwaka mmoja wa utekelezaji wa programu ya m-mama inayotoa huduma ya usafiri wa dharura na rufaaa kwa wajawazito na watoto, mkoa wa Arusha umefanikiwa kupunguza vifo 19 kutoka vifo 67 mwaka 2022/23 na kufikia vifo 48 mwaka 2023/24 sawa na 28.3%.
Akizungumza wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi, kufungua kikao kazi cha mwaka cha Tathmini ya utekelezaji wa mfumo wa huduma ya M - mama mkoa wa Arusha, kilichofanyika kwenye hoteli ya Corridor Spring Jijini Arusha mapema leo Julai 30, 2024, Kaim Mganga Mkuu Mkoa wa Arusha, Dkt. Edna Chonge Ntulle ameweka wazi kuwa, kwa kipindi cha mwaka mmoja na miezi mitatu ya programu ya M- mama imefanya mageuzi ya kupunguza vifo vya wajawazito na watoto.
Amesema kuwa, katika mkoa wa Arusha, mfumo wa m-mama ulifunguliwa mwaka 19.12 2022 na kuanza utekelezaji wake Machi 2023, kwa kipindi hicho mkoa umefanikiwa kupunguza vifo vya wajawazito na watoto kwa asilimia 28.3.
"Kupitia m-mama tumefanikiwa kusafirisha wajawazito na wazazi 4,189 sawa na asilimia 82, Watoto wachanga 808 sawa na asilimia 18 na kufanya juma ya rufaa zilizoingizwa kwenye mfumo kuwa 4,997 sawa na asilimia 92.
Ameweka wazi kuwa, lengo ya kikao kazi hicho ni kufanya tathmini ya utekelezaji wa mfumo wa m-mama ili kutambua changamoto halisi na kuweka mikakati na utatuzi endelevu ya ili kupungu kuondoa kabisa vifo visivyo vya lazima.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.