• Complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Arusha Regional

The United Republic of Tanzania President Office Regional Administration and Local Government Arusha Regional

  • Home
  • About Us
    • History
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa mikoa waliopita-Arusha
    • Dira na dhima
    • The basics
    • Strategies
  • Administration
    • Structure
    • Departments
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Units
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • District
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Councils
    • Arusha CC
    • Arusha DC
    • Meru DC
    • Monduli DC
    • Karatu DC
    • Longido DC
    • Ngorongoro DC
  • Investment Opportunities
    • Tourism
    • Livestock
    • Agricultre
    • Industrial
  • Our Service
    • Health
    • Education
    • Water
    • Land
    • Tourism
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

RAIS DKT. SAMIA AMEDHAMIRIA KUWAINUA WANAWAKE- WAZIRI DKT.GWAJIMA....

Posted on: October 16th, 2023

Na Prisca Libaga  


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuwainua wanawake kiuchumi kwa kuweka msingi unaochochea mabadiliko yanayojielekeza kukua kiuchumi.


Hayo yamesemwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima wakati wa Maadhimisho ya Kimataifa ya Siku ya Mwanamke anayeishi Kijijini yaliyofanyika Oktoba 15, 2023 kwenye Kijiji cha Olevolosi, Kata ya Kimnyak, Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha.


Waziri Dkt. Gwajima ameelezea nia ya Rais Dkt. Samia kuwainua Wanawake kwa kutaja baadhi ya mambo yanayotekelezwa na kuwagusa wanawake kwa kurejea takwimu, ikiwemo mikopo ya Sh. bilioni 713.8 iliyotolewa Julai 2022 hadi Machi, 2023 ambapo, imezalisha ajira 3,122,104 huku wanawake wakiwa 52%. Aidha, amesema mikopo hiyo ilienda kwa wajasiriamali 2,203,838 ambapo wanawake ni asilimia56


Kwa upande wa kilimo ambako wanawake wengi ndiyo nguvu kazi Dkt Gwajima amesema, Serikali imewezesha Ruzuku kwenye mbolea ambapo sasa bei ni Shilingi 73,468 badala ya Shilingi 109,000 kwa mfuko wa kilo 50 kupitia wakala waliopitishwa na Serikali katika ngazi za vijiji kwa mwaka 2023.

Vilevile, Serikali Kupitia mfuko wa pembejeo wa Taifa imetoa mikopo ya pembejeo za kilimo, mifugo na uvuvi.


Kwa upande wa mwanamke na ardhi amesema idadi ya wanawake wanaomiliki ardhi imekuwa ikiongezeka ukilinganisha na awali ambapo kufikia 2021/22 jumla ya Hatimiliki za Kimila 1,171,884 zimetolewa huku wanawake wakiwa 406,915.


Kuhusu biashara ya mazao ya kilimo, Dkt Gwajima amewaasa Wanawake kufanya biashara kwa kuongeza mnyororo wa thamani kwenye mazao ya kilimo na pia, kuhakikisha bidhaa zina alama ya msimbomlia (barcode), vifungashio nadhifu na vyenye ubora ili kukidhi vigezo kwenye masoko makubwa ya ndani na nje ya Tanzania,


“Nimefurahi kuona sabuni kutoka kwenye zao la asali kwenye moja ya mabanda niliyotembelea yaani zao la asali limeongezwa thamani” Dkt. Gwajima.


Kuhusu masoko, Waziri Dkt. Gwajima amewaasa wanawake kutumia fursa ya kidijitali kwa kufungua maduka ya kidijitali ili kutangaza bidhaa zao, kwani idadi ya watu wanaoona bidhaa mtandaoni ni kubwa na kwa muda mfupi.


Waziri Dkt Gwajima, ametumia fursa hiyo kuhamasisha wanawake kujiunga na majukwaa ya uwezeshaji kiuchumi


“Tunayo majukwaa ya uwezeshaji wanawake kiuchumi lakini wengi hawajajiunga hivyo, Maafisa Maendeleo hakikisheni mnatoa elimu ya kutosha kwa Wanawake, hususan wa kijijini,” amehimiza Waziri Dkt. Gwajima.


#arushafursalukuki

#KaziInaendelea



Announcements

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • View All

Latest News

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • View All

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
More Videos

Quick Links

  • Guildlines Towards the use of ICT In Government
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Public Servant Portal
  • Takwimu
  • TANAPA

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap
    • FAQ

Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.