Kwaniaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda amekabidhi gari mpya chapa ya Land Rover Discovery yenye Thamani ya Milioni 100 kwa Sheikh wa Mkoa wa Arusha Sheikh Shaaban Bin Juma ili kuweza kumsaidia kwenye shughuli zake za kidini Mkoani hapa.
Mhe. Paul Makonda amekabidhi gari hilo muda mchache baada ya kumalizika kwa sala ya Ijumaa kwenye msikiti Mkuu wa Bondeni Jjjini Arusha leo Oktoba 25, 2024, akiwataja Viongozi wa dini kama msingi mkuu wa amani na utulivu unaoshuhudiwa kote nchini Tanzania.
Kwa Upande wake Sheikh Shaaban Bin Juma baada ya kukabidhiwa gari hilo, amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Upendo wake kwa Watanzania, akimuombea Kheri Rais Samia pamoja na wasaidizi wake katika kuwatumikia wananchi wa Tanzania.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.