Na Elinipa Lupembe
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekabidhiwa rasmi Mwenge wa Uhuru 2023 kutoka kwa Kiongozi wa Mbio hizo Ndugu Abdallah Shaibu Kaimu wakati wa Maadhimisho ya Kilele cha mbio hizo yaliyofanuika kwenye uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati Mkoani Manyara leo tarehe 14 Oktoba, 2023.
Mwaka 2023 Mwenge wa Uhuru umekimbizwa mikoa 31 ya Tanzania Bara na visiwani na kitembelea, kukagua, kuweka mawe ya msingi, kufungu na kuzindua miradi ya Maendeleo kwenye halmashauri 186
Mwenge wa Uhuru 2023 uliobeba kauli mbiu ya Tunza Mazingira, Okoa vyanzo vya maji, kwa Ustawi wa Viumbe Hai, kwa Uchumi wa Taifa, umehitimisha rasmi mbio zake tarehe 14.10.2023.
#ARUSHAFURSALUKUKI
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.