Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Missaile Albano Musa, amezindua Msimu wa Wiki ya Huduma kwa wateja benki ya CRDB Kanda ya Kaskazini ulifanyika katika tawi la benki hiyo mkoani Arusha, Oktoba 07,2024.
Katibu Tawala huyo, ameipongeza Benki ya CRDB kwa abunifu mkubwa unaokwenda sambamba na kuwapa kipaumbele wateja wao, katika bidhaa na huduma mbali mbali wanazozitoa.
Kipekee amepongeza huduma ya Chatbot ijulikanayo kama *Elle* kwani ni njia sahihi itakayowarahisishia wateja kupata huduma kwa wakati.
Akizungumza kwa niaba ya Benki, Kaimu Meneja wa Kanda Bw. David Peter amesema benki ya CRDB inatumia wiki hii kusherekea wateja na kuwapongeza wafanyakazi wanaotoa huduma bora kwa wateja.
Uzinduzi huo uliudhuriwa na Bi Mary Kimasa Meneja wa Tawi la Arusha, Wateja na wadau mbali mbali pamoja na Wafanyakazi wa Benki ya CRBD Arusha.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.