Mkuu wa Mkoa wa Arusha Iddi Hassan Kimanta, ametoa wito kwa vyama vya Michezo Mkoani Arusha kuandaa timu zao vizuri ili ziwezi kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali.
Pia ametoa wito kwa wanamichezo kuwa wapende kuangalia zaidi sifa wanazozileta katika nchi kuliko sifa zao binafsi.
Ametoa wito kwa Makocha kuzingatia kupata elimu ya kutosha katika Michezo wanayofundisha ili waweze kutoa wachezaji bora zaidi.
Hayo ameyasema alipokuwa akikabidhi zawadi mbalimbali kwa washindi wa tamasha la Michezo ya Olimpiki,Wilayani Karatu.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.