Na Elinipa Lupembe
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda amemuagiza Mkuu wa Polisi wa Usalama Barabarani Mkoani humo, kutokuyakamata magari ya Utalii yakiwa yamebeba wageni, badala yake ukaguzi wa magari hayo ufanyike kabla ya kupakia watalii na ufanyike kwenye mipaka na viwanja vya ndege vinavyotumiwa na watalii.
Mhe.Makonda ametaoa maagizo hayo wakati akizungumza waandishi wa habari kwenye Viwanja vya Magereza Kisongo, wakati wa maonesho ya kimataifa ya Utalii ya Karibu - Kili Fair 2024, Juni 08, 2024, maonesho yaliyojumuisha makampuni zaidi ya 460 ya kimataifa kutoka kwenye mataifa zaidi ya 50.
Amesisitiza kuwa, nivema Jeshi la Usalama Barabarani kuwa na utaratibu wa kufanya ukaguzi wa magari ya utalii kabla wageni hawajapanda, ili kuruhusu magari hayo kufanya safari zao bila kusimamishwa na kubughudhiwa na Askari wawapo barabarani, na kuagiza kutokusimamisha magari hayo yakiwa yamebeba watalii.
"Kwa kufanya hivyo kutasaidia kutowapotezea muda watalii wawapo njiani suala ambalo litawapa muda zaidi wa kuwepo kwenye hifadhi za utalii na sehemu nyingine, pamoja na kuwaongeza muda wa matumizi ya fedha,bidhaa na huduma nyingine zinazopatikana Arusha na hivyo kuingizia mkoa fedha nyingi zaidi za kigeni".Amesisitiza Mkuu huyo wa Mkoa
Hata hivyo Mhe. Makonda ametoa miezi miwili kwa wamiliki wa Teksi zinazotumika kubeba wageni na watalii wa Mkoa humo kuwa na rangi maalumu za kufanana, kuwarahisishia watalii kuyatambua na kulifahamu gari husika na kwa usalama zaidi kwa wageni wanapoamua kutumia aina hiyo ya usafiri wawapo Arusha.
Awali, amekiri kuendelea kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan za kuvitangaza vivutio vya Utalii vinavyopatikana Tanzania pamoja na ukarimu wa Watanzania, huku akitaka kila mwanaArusha kwenye eneo lake la kazi kuonesha ukarimu huo kwa vitendo kila wanapokuwa wanahudumia wageni. @baba_keagan
@ortamisemi
@polisi.tanzania
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.