RC MAKONDA AAPA KUSHUGHULIKA NA WASAIDIZI WAKE WANAOKWAMISHA MAENDELEO MKOANI ARUSHA.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda amesisitiza Matokeo chanya kwa kila kinachofanywa na Watumishi wa Umma Mkoani Arusha, akisema hilo ndilo suala pekee la kuonesha dhamira ya dhati katika kumuunga Mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan badala ya kutanguliza Upambe na majungu kwenye maeneo yao ya Kazi.
Mhe. Makonda ametoa kauli hiyo mapema Leo Jumatano Oktoba 16, 2024, wakati akizindua kampeni ya Mtaa kwa Mtaa, inayosimamiwa na Mamlaka ya Maji na usafi wa Mazingira Jiji la Arusha AUWSA ikilenga kukuza mtandao wa Maji kwenye Kata 25 zenye mitaa 154, inayopatikana ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Arusha mkoani Arusha.
Mhe. Paul Christian Makonda katika hatua nyingine amewaahidi wananchi wanufaika wa mradi huo wa Maji kuwa atahakikisha usiku na mchana miradi yote inafanikiwa na kutoa huduma kwa wananchi, akikosoa ucheleweshaji wa miradi mingi ya maendeleo kutokamilika kwa wakati na kutokuwa na tija iliyodhamiriwa na serikali.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.