Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda leo Septemba 25, 2024 jijini Arusha, amekutana na kuzungumza na Bodi na Uongozi wa Chuo cha Taifa cha Utalii akiwasihi kuongeza jitihada katika kukuza uelewa wa sekta ya utalii kwa Watanzania.
Mhe. Makonda amekutana na Mkuu wa chuo cha Taifa cha Utalii Dkt.Florian George Mtei, Mwenyekiti wa bodi Bw. Imani Kajula, Makamu Mkuu wa chuo Taaluma, tafiti na Ushauri Bi. Jesca William, Makamu mkuu wa chuo, fedha na Mipango Bw. Kakulima Munguabela na Meneja wa Kampasi ya Arusha Dkt. Maswet Masinda.
Katika mazungumzo yao Mhe. Makonda amezungumzia pia changamoto ya huduma kwa wateja kwenye sekta ya utalii, akikitaka chuo hicho kusimamia ubora wa huduma kwenye hoteli zinazohudumia watalii wanaokuja nchini Tanzania pamoja na kuanzisha klabu za Utalii mashuleni ili kukuza uelewa wa pamoja kuhusu utalii.
Kwa upamde wake Mwenyekiti wa bodi ya chuo hicho Bw. Imani Kajula, amempongeza Mhe. Makonda kwa kutekeleza kikamilifu maelekezo ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu utalii wa Arusha,akimuomba kuendeleza jitihada zake katika sekta hiyo muhimu kwa uchumi wa Arusha
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.