Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda amewataka wafanyabiashara na wawekezaji wa Mkoa wa Arusha kutumia kikamilifu ugeni wa Maafisa na watendaji mbalimbali wa serikali wanaofika Mkoani Arusha kwa shughuli mbalimbali za kiserikali na binafsi.
Mhe. Makonda ametoa kauli hiyo leo jioni Agosti 29, 2024 wakati akizungumza na Watendaji na Wenyeviti wa Taasisi, mashirika na Wakala za serikali pamoja na wafanyabiashara wa Mkoa wa Arusha, walipokutana kwenye hafla maalum ya kubadilishana uzoefu na kufahamiana kwa lengo la kukuza na kustawisha biashara na uchumi wa Arusha.
"Tuitumie fursa hii ili kufahamiana na Viongozi wetu na mahusiano haya yanaweza kuibadilisha Arusha na ukawa ni mkoa wenye wafanyabiashara wanaojivunia serikali yao kwa kuwa karibu yao kwenye nyakati zote." Amesema Mhe. Paul Makonda.
Wenyeviti wa bodi na Watendaji wakuu wa Taasisi za Umma waliopo Arusha kwenye Mkutano wao wa Mwaka, wamekutana na wafanyabiashara hao ikiwa ni wazo la Mkuu wa Mkoa wa Arusha katika jitihada zake za kulea na kustawisha uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na uchumi wa mkoa.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.