Na Elinipa Lupembe
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Christian Makonda amemshukuru mama Halima Hzmad, aliyetoa eneo kwa ajili ya kupisha ujenzi wa Kituo cha afya kata ya Bwawani, halmashauri ya Arusha, wilaya ya Arumeru.
Mhe. Makonda ametoa shukurani hizo, mara baada ya kupokea taarifa ya ujenzi wa kituo cha Afya Bwawani, kilichojengwa na Serikali kupitia Mfuko wa Mandeleo ya Jamii - TASAF kwa gharama ya shilingi milonimiloni, alipotembelea kukagua mradi huo Mei 28, 2024.
Amempongeza mama huyo, kwa moyo wake wa uzalendo na kujali wengine kwa kutoa eneo lake kwa ajili ya kuhudumia watu takribani elfu 14 na kumuombea kwa Mungu ambariki na akumbuke sadaka yake
"Ninamshukuru sana mama Halima kwa kukubali kutoa eneo lake, sadaka hii ya thamani, Mungu aikumbuke kila atakayepona kwenye kituo hiki, ukapone wewe na uzao wako kama ilivyobarikiwa sadaka ya Abraham" Amesema Makonda
Aidha, ameipongeza Serikali ya awamu ya sita kwa jitihada zake za kuhakikisha huduma za afya zinasogezwa karibu na wananchi hususani ameneo ya pembezoni kama ilivyo kata ya Bwawani na kuonheza kuwa Serikali ya mama Samia inawajali watanzania wote na kuhakikisha wanapata huduma bila kujali umbali wa maeneo wanayoishi.
"Serikali ya awamu ya sita imehakikisha wananchi wanapata huduma karibu na maeneo wanayoishi, jambo ambalo linawapunguzia mzigo wa kutembea umbali mrafu pamoja na kupunguza gharama za usafiri pia.
Hata hivyo, mama Halima kwa niaba ya wananchi wa kata ya Bwawani, amemshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan na kumuomba Mkuu wa Mkoa huyo, kufikisha zawadi ya kuku kwa Mama Samia kama ishara ya shukurani na upendo kwa namna alivyowathamini kwa kuwajengea kituo cha afya.
"Kata yetu haikuwa na kituo cha afya miaka mingi, mama Samia ameona umuhimu wetu na kutujengea Kituo cha afya, ametusaidia sana sisi wanawake wa Bwawani na familia zetu, tunakuomba mkuu wetu wa mkoa mpe salamu zetu mama Samia". Amesema Mama Halma
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.