_Aahidi kusimamia na kutekeleza maelekezo yake_
Akimkaribisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda amemtaja Mhe. Mchengerwa kama kiongozi anayefikika na mwenye umahiri mkubwa katika kuwatumikia wananchi.
"Hakuna wizara ulishawahi kwenda ikapoa,Umeenda kwenye michezo kule umetuwekea alama kwenye Utumishi pia umefanya kazi nzuri na hata zile wizara unazojua kwamba hazina mambo kumbe zina mambo, inategemea tu mtu na mtu.Haya mambo yanategemea nani amekaa,unaweza ukawa hata Mwenyekiti wa mtaa watu wasijue kama upo lakini kuna mtu akikaa watu wanajua kuna mtu pale." Amesema Mhe. Makonda.
Katika hatua nyingine Mhe. Paul Christian Makonda amemuahidi Mhe. Mchengerwa kusimamia maelekezo yote aliyoyatoa kuhusu uchaguzi ujao wa serikali za mitaa, ikiwemo kuhakikisha kuwa wananchi wa Tarafa ya Ngorongoro wanashiriki uchaguzi huo kikamilifu kulingana na sheria na miongozo iliyopo.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.