Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda akiotesha mti mbele ya Jengo la Ofisi mpya za Makao Makuu ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongo (NCAA), alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi hizo wakati wa ziara yake ya kikazi wilayani Karatu mapema leo Mei 24, 2024
Katika ziara hiyo maarufu kama 'Siku 6 za Moto Arusha' , Mhe. Makonda amekagua shughuli za maendeleo ikiwemo utekelezaji wa miradi ya maendeleo kisekta pamoja na kuzungumza na wananchi kwenye mkutano wa Hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Mazingira Bora.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.