RC MAKONDA APOKELEWA OFISI ZA CCM MERU, TAYARI KUENDELEA NA ZIARA YAKE
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda amefika katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Meru (Kichama) ambapo amepokelewa na Mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo Ndugu. Ndewirwa S. Mbisse mapema leo Mei 29, 2024
Mhe. Makonda amefika ofisini hapo kama ilivyo utaratibu wa kawaida kabla ya kuanza ziara kuripoti katika ofisi za chama katika wilaya husika na ikiwa ni wilaya ya tano kati ya 6 anazotarajiwa kuzitembelea kwenye ziara yake ya kikazi ya SIKU 6 ZA MOTO ARUSHA ambapo leo ni siku ya tano.
#ArushaNaUtalii
#ArushaYaSamia
#Siku6ZaMoto
#KaziIendelee
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.