Akizungumza na maelfu ya Wananchi wanaohudhuria Kongamano kubwa la Operesheni Washa Taa linaloratibiwa na Mtume Boniface Mwamposa wa Kanisa la Inuka Uangaze, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda amewataka watanzania kuwakataa watu wanaotumia Neno la Mungu na mavazi rasmi ya Viongozi wa dini katika kuwarubuni Watanzania na kujinufaisha kupitia maandiko matakatifu.
"Ukimuona mtu yeyote mwenye jina au nafasi yoyote ya kidini lakini umaarufu wake hautokani na kazi ya mikono ya Kristo, hautokani na kazi za Mungu na za neno la Mungu, jua huyo ni Kiongozi wa dini feki. Nikupe mfano unielewe, Apostle Mwamposa hapa kamtaja Yesu Mwanzo mpaka mwisho, mmejaa hapa mnashuhudia kazi za neno la Mungu kupitia kinywa cha Mtumishi wake aliyepakwa mafuta kwaajili ya nyakati hizi, Heshima aliyonayo ni ya kufanya kazi ya Mungu ambayo sisi ni mashuhuda wa Matunda na maandiko yanasema mtawajua kwa matunda yao." Amesema Mhe. Makonda.
Mhe. Makonda amewaambia watanzania kuwa kumekuwepo na lindi kubwa la wanaojiita watumishi wa Mungu sasa hivi wakiwa na ukwasi na majina maarufu lakini umaarufu wao hautokani na kazi ya Uponyaji na kazi za mikono ya Kristo kama ambavyo kanuni zinazungumza kuhusu wakristo na Ukristo ulimwenguni kote.
Katika kudhihirisha uhakika wa kile alichokizungumza, Mhe. Paul Christian Makonda amealika na kuwakaribisha watu wanaohitaji mjadala naye kuhusu Ukristo, namna inavyotakiwa maisha ya mkristo kuwa pamoja na namna mbalimbali ambazo Mungu ameagiza na kuelekeza Wakristo katika utatuzi wa changamoto za kijamii na namna wanavyotakiwa kuishi wao pamoja na Viongozi wao wa kidini.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.