Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda, ametangaza kuanza kwa siku tatu maalumu za Haki, ambazo atazitumia kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi wa mkoa wa Arusha, kuanzia Jumatano ya wiki ijayo Tarehe 08 - 10 Mei, 2024.
Akizungumza na Mhe. Makonda amesema kuwa hatua hiyo ni utekelezaji wa maagizo ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na ahadi yake aliyoitoa kwa wakazi wa Arusha Aprili 09, 2024 wakati alipowasili kwenye kituo chake cha Kazi na kukabidhiwa ofisi na Mtangulizi wake Mhe. John Mongella.
Mhe. Paul Christian Makonda amesema tayari ameandaa taasisi zote za mkoa wa Arusha pamoja na Wanasheria wabobezi kwenye mashauri mbalimbali, akiahidi pia kutoa bure Wanasheria ili kuwasimamia wananchi watakaokuwa na mashauri yatakayokuwa na uhitaji wa kupelekwa mahakamani.
Zoezi hilo la kusikiliza na kutatua kero za wananchi litafanyika kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, ambapo Mkuu wa Mkoa amewahakikishia wakazi wa Arusha kuendelea kuwa sauti na sikio la Wanyonge kwa kuhakikisha waliodhulumiwa na kukandamizwa, wanapata haki zao kwa msaada wa ofisi yake.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.