Na Elinipa Lupembe
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda akiwasili kwenye shule ya Sekondari Madiira, kata ya Sing'isi halmashauri ya Meru, wilaya ya Arumeru na kupokelewa na wanafunzi wa shule hiyo.
Mhe. Makonda amefika shuleni hapo kwa ajili ya kutemblea na kukagua mradi wa ujenzi wa shule hiyo mpya iliyojengwa na Serikali kufuatia Mpango wa Kuboresha miundo mbinu ya shule za Sekodnari nchini SEQUIP kwa gharama ya shilingi milioni 584.2, fedha zilizojumuisha majengo yote muhimu ya shule ikiwemo vyumba vya madarasa, jengo la utawala na ofisi za wamimu, maabara za masomo yote ya Sayansi Fizikia, Kemia na Baiolojia, Maktaba, Chumba cha TEHAMA pamoja na vyoo vya walimu na wanagunzi.
Hata hivyo, Mhe. Makonda amewapongeza wasimamizi wa mradi huo ambao umekamilika na tayari wanafunzi wameanza masomo shuleni hapo kuanzia Januari, 2024 na kuwasisitiza walimu kuwasimamia wanafunzi kusoma kwa kuwafundisha taaluma na maadili mema ya nchi yetu.
Aidha, amewataka wanafunzi kutambua fursa waliyopewa na serikali yao pendwa ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye anapambana kuhakikisha watoto wote wa kitanzania wanapata elimu kwenye mazingira bora karibu na maeneo yao.
"Serikali imewekeza kwenu wanafunzi ili kupata watalamu wa fani mbalimbali za kulitumikia Taifa lenu, najua kila mmoja anayo ndoto yake, elimu mnayoipata shuleni hapa iwape ujezi na maarifa ya kutimiza ndoto zenu huku mkitangulie nidhamu na uzalendo kwa ajili ya nchi yenu" Amesisitiza Mhe. Makonda
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.