Na Elinipa Lupembe
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt. Emmanuel Nchimbi, amemteua Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda kuwa Mlezi wa Shina la wakereketwa na Wajasiriamali wa Chama Cha Mapinduzi wa kata ya Makuyuni wilaya ya Monduli Juni 02,2024.
Katibu Mkuu huyo ameteua Mhe.Makondq mara baad aya kuzindua shina hilo la wakerketwa Wajasiriamali na baadaye kuhutumbia wananchi wa Monduli eneo la Makuyuni na kusikiliza kero za wananchi.
Dkt. Nchimbi na timu yake wapo kwenye ziara ya kikazi ya siku tatu ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Arusha kuanzia tarehe 02 -4 Juni, 2024 ambapo atatembelea wilaya ya Monduli, Wilaya ya Arusha mjini na wilaya zakichama Arumeru na Meru.@nchimbie @baba_keagan @ccmtanzania @ccmmkoaarusha @ccm_arumeru_2022_2027 @uvccm_tz
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.