Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda amewashukuru wananchi wa mkoa wa Arusha kwa kuendelea kuunga mkono shughuli zote za maendeleo zinazotekelezwa kwenye Mkoa huo, ambao ni dhahiri wanamuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Ametoa shukurani hizo wakati akiwasilisha Ripoti ya miezi sita mbele ya waandishi habari, Mkutano uliofanyika kwenye kituo cha mikutano ya kimataifa Arusha AICC ukumbi wa Simba, leo Novemba 17, 2024
Amesema kuwa, Maendeleo ya Mkoa wa Arusha yanategemea afya ya wananchi na amani, ninasisitiza kuilinda amani yetu hasa tunapokwenda kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa tukafanye chaguzi kwa amani na utuliivu.
"Ninawasihi wanaarusha tuilinde amani yetu, tusikubali kugawanywa kwa namna yoyote ile, maendeleo ya kijamii na kiuchumi tunayoyapata ni kutokana na amani tuliyonayo, tusikubali kuvurugana kwa maslahi ya watu wachache" Amesema Mhe. Makonda.
Mhe. Makonda, amewaahidi wananchi utumishi uliotukuka kwa kufanya kazi usiku na mchana kwa ajili ya kuwahudumia wananchi huku akimtaka kila mtu atimize wajibu wale, na kufafanua kuwa, Serikali inatimiza wajibu wake, wananchi pia watimize wajibu wao na zaidi watumishi wa Umma waendelee kutimiza wajibu wao wa kuwahudumia wananchi ili kufikia maelengo ya Serikali ya awamu ya sita.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.