Na Elinipa Lupembe
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda, amewasili wilaya ya Longido na kupokelewa na Mkuu wa wilaya hiyo Mhe. Marco Ng'umbi ofisini kwake mapema leo Mei 23, 2024 na kuwataka viongozi na watumushi kuwajibika na kutambua kuwa kipaumbele chake ni kazi.
Mhe. Makonda yuko wilayani Longido, ikiwa ni zara yake ya kwanza ya kikazi ya kutembelea wilaya za mkoa wa Arusha, na kukutana na viongozi wa Chama, Serikali, Jamii na Watumishi wa Wilaya hiyo na kuweka wazi kuwa, amefika wilayani humo licha ya kufanya shughuli za kikazi ni fursa yake ya kipekee ya kufahamiana pamoja na kuangalia namna ya utendaji kazi wa viongozi na watumishi katika kuhudumia wananchi.
Amewataka viongozi na watumishi wote kutambua dhamana kubwa waliyoibeba ya kuwahudumia wananchi na kutojishahau, badala yake kuheshimu dhamana hiyo kwa kufanya kazi huku wakitambua kipaumbele chao pekee ni kazi na si vinginevyo.
" Viongozi na Watumishi wetu wafahamu, kila mmoja kwa nafasi yake anapaswa kutambua wananchi ndio 'maboss' wetu ambao wametuajiri na kutuweka madarakarakani, hivyo ni vema kila mtu kutekeleza majukumu yake na kuhakikisha wananchi wanahudumiwa ipasavyo" Amebainisha Mhe.Makonda
Hata hivyo, ameweka wazi matamanio yake ni kuona wananchi wanatambusa kuwa, Serikali ya awamu ya sita chini ya Jemadari Dkt. Samia Suluhu Hassan inawathamini sana hivyo, watumishi waliopewa dhamana yananalo jukumu la kutimiza wajibu wao ndio heshima ya utumishi wa Umma.
"Mwananchi anatakiwa kujisikia fahari kuhudumiwa na Serikali yake pendwa, huku akitambua huduma za kijamii zilizoletwa na Serikali kwenye eneo lake ni kazi kubwa ya Dkt.Samia"
Amewakumbusha Waheshimiwa Madiwani kupitia Baraza lao, wanayo dhamana kubwa kwa kuwa wao ni wawakilishi wa wananchi hivyo jukumu lao ni kuhakikisha, wanashughulikia kero za wananchi kwa kuzibeba na kuziwasilisha kwenye vikao halali vya halmashauri ili ziweze kutafutiwa ufumbuzi.
"Dhamana ya uongozi mliyopewa ni kuwahudumia wananchi"
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.