Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda amesema amedhamiria vilivyo kulea na kukuza vipaji vya wananchi wa Arusha, akiahidi kuwa na programu mbalimbali za kutambulisha vipaji vya wananchi wa Mkoa wa Arusha
Mhe. Makonda ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na washiriki wa mashindano ya pikipiki ya Samia Motocross Championship, na kuwaalika wananchi wote kuweza kuhudhuria mashindano hayo yanayofanyika Jumapili hii Julai 14, 2024 kwenye viwanja vya Lakilaki Kisongo.
"Mmefanya sana mazoezi na mashindano na mwisho yakaonekana kama ni mashindano ya kawaida na ya kitoto sasa nataka kuwaambia watu wazima tumeingia kwenye Game.Lazima heshima iwepo.", amesema.
Katika hatua nyingine Mhe.Makonda amesisitiza kuwa ataendelea kuwawezesha washindi mbalimbali watakaotokana na mashindano hayo ya pikipiki ili waweze kuiwakilisha Tanzania kwenye michuano mbalimbali ya kikanda na kimataifa ikiwemo mashindano yatakayofanyika mwezi wa tisa nchini Morocco.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.