Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda Paul Makonda ametangaza kutoa lita 20,000 za Mafuta ya Petroli na Dizeli kila mwezi kwa Taasisi za ulinzi mkoani humo, ikiwa ni jitihada na mkakati wa kuongeza kasi na ufanisi katika kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao..
Mhe. Makonda ametangaza kutoa kiasi hicho cha mafuta, wakati wa kikao kazi na Wakuu wa Taasisi za Ulinzi mkoa wa Arusha na Mhe. Makonda, kikao chenye lengo la kufahamiana na kuangalia namna ya taasisi hizo kufanya kazi pamoja kama timu, kilichofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano, ofisi ya mkuu wa mkoa huo Julai 11, 2024,
Amesema kuwa ametoa kiasi hicho cha mafuta ili kuwahudumia wananchi, huku akiweka wazi kuwa, kufikia Mwezi Agosti hatapenda kusikia wananchi wanakosa kuhuduma, kwa kuwa tayari ameviwezesha vyombo hivyo vindea kazi muhimu ikiwemo mafuta, pikipiki na magari ya zimamoto, Vyombo vingine vya ulinzi na usalama.
Katika Mgao huo, Jeshi la Polisi limepatiwa lita 12,000, Jeshi la uhamiaji Lita 2,000, Zimamoto na Uokoaji Lita 1,000, Magereza Lita 1,000 pamoja na lita 1,000 ambazo zimegaiwa kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ.
Hata hivyo, Mhe. Makonda ametangaza kupokea pikipiki nyingine 110 kutoka kwa wadau mbalimbali wa maendeleo, walioamua kutoa pikipiki hizo ili kuunga mkono jitihada za kuimarisha ulinzi na usalama Mkoani Arusha ili kuvutia shughuli za kiuchumi pamoja na utalii.
"Nafasi niliyopewa nimepewa na Dkt. Samia kupitia mapenzi ya Mungu na jukumu langu ni kutumia mazingira niliyonayo kuongeza ufanisi wa watendaji waliopo kwenye nafasi zilizopo chini yangu ili kwa pamoja tuwe na matokeo mazuri yanayoweza kuleta utoaji mzuri wa huduma kwa wananchi lakini pia heshima kwa Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyetupa nafasi ya kumuwakilisha." Ameongeza Mhe. Makonda.
Halikadhalika pia Mhe.Paul Christian Makonda ametangaza utaratibu mpya wa kutoa kahawa na maziwa kwa vituo vyote vya ukaguzi na utendaji wa vyombo vya ulinzi na usalama ikiwemo vituo vya Polisi vinavyofanya kazi nyakati za usiku kwenye mkoa wa Arusha ili kuongeza chachu katika kuwatumikia wananchi wa mkoa wa Arusha.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.