Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Makongolo Nyerere amefunga maonesho ya nanenane Kanda ya Kaskazini huku akiambatana na wakuu wa Mikoa ya Arusha Mhe.John Mongella na Mhe. Nurdin Babu wa Kilimanjaro.
Katika kilele cha maadhimisho hayo viongozi wengine mbalimbali walihudhuria wakiwemo Makatibu Tawala wa Mikoa, wakuu wa Wilaya, wakurugenzi,wenyeviti wa halmashauri na viongozi kutoka taasisi za serikali kutoka Mikoa yote mitatu.
Zaidi ya waoneshaji 300 wameweza kutoa elimu mbalimbali juu ya Kilimo, ufugaji na uvuvi kwa wananchi waliofika katika maonesho hayo.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.