Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. John V.K Mongella amewataka wakuu wa wilaya na Wakurugenzi wa halmashauri za mkoa wa Arusha kuwajibika kusimamia ajenda ya lishe kwenye maeneo yao, ili kuokoa kizazi cha watanzania na kurahisisha utekelezaji wake.
Mhe. Mongella ametoa agizo hilo wakati wa kikao cha Tathmini ya Lishe mkoa wa Arusha, chenye lengo la kufanya Tathmini ya lishe ngazi ya mkoa, kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano Ofisi ya Mkuu wa mkoa huo, leo tarehe 12 Februari, 2024.
Amesema kuwa, kutokana na unyeti wa suala la lishe nchini na Mheshimiwa Rais akiwa ndio Championi wa agenda ya Lishe nchini, hivyo kila Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi kuhakikisha ameibeba na kuiishi katika maisha yake ya kazi ili kuhakikisha wananchi wanakuwa na lishe bora.
Licha ya kuwa kuna mabadiliko na maendeleo katika suala la Lishe, bado tuna kwenda taratibu, wakati lishe ni msingi wa maisha ya binadamu, ajenda ya lishe haina mbadala, ni agenda nyeti na muhimu katika mustakabali wa Taifa, ili taifa letu liweze kuendelea linahitaji wananchi wenye lishe bora ambao wana uwezo wa kufikiri na kufanya kazi kwa maendeleo ya taifa hili la Tanzania
"Kila kiongozi kwenye eneo lake ahakikishe anafuatilia utekelezaji wa afua za lishe, Wakuu wa wilaya msiifanye ajenda ya lishe kama ni kutekeleza mkataba mliousaini, wala wakurugenzi msitoe hela kwa kuwa mnalazimishwa, fuatilieni utekelezaji wa afua za lishe katika maeneo yenu" Amesisitiza Mhe.Mongella.
Hata hivyo, akiwasilisha taarifa ya Tathmini ya alishe kwa kipindi cha kuanzia mwezi Julai - Desemba, 2023, Afisa qlishe Mkoa wa Arusha, Doto Milembe, amesema kuwa hali ya utoaji na upatikanaji elimu ya lishe imeongezeka, hali yauoatikanaji chakula cha wanafunwzi shuleni imefikai asilimia 87, huku halmshauri zikiavuka malengo ya fedha zilizopangwa kwenye bajeti ya mwaka
Amesisitiza kuwa, kikao hicho ni maalum kwa ajili ya kuainisha na kujadili viashiria ambavyo havijatekelezwa kwa ufanisi na kuweka mikakati ya kuboresha utekelezaji wa mkataba wa afua za lishe, hivyo suala la Lishe ni mtambuka hivyo, watalamu wa ngazi zote kushirikiana na watoa huduma ngazi ya jamii kutoa elimu ya lishe na kusisitiza kuwa lishe bira ianze na wadau watalam husika.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.