Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. John V.K Mongella, ameuagiza uongozi wa wilaya ya Longido kupitia Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji, kuchukua hatua za haraka kujenga chumba cha kuhifadhia maiti (mochuari) kwenye kituo cha Afya Ketumbeine, kituo ambacho kimejengwa na fedha kutoka Serikali kuu, zaidi ya shilingi milioni 500.
Mhe. Mongella ametoa agizo hilo mara baada ya wananchi wa Ketumbeine, kulalamikia uwepo wa changamoto hiyo, unaowalazimu kutumia gharama kubwa kwenda kuwahifahi wapendwa wao, Longido mjini umbali wa Km 90 mpaka 120, wakati wa mkutano wa Hadhara, uliowakutanisha wakazi wa Tarafa ya Ketumbeine, kwenye kijiji cha Lopolosek.
"DC na Mkurugenzi, tusisubiri kila kitu kufanyiwa na Serikali Kuu, wametoa fedha za kukamilisha Kituo cha Afya, tumieni mapato ya ndani kujenga chumba cha mochuari, sio lazima kusubiri kila kitu kusubiri kufanyiwa na Serikali Kuu, jiongezeni, ninawapa mwezi mmoja, nitakuja kugungua mochuari hiyo" Mhe Mongella
Awali, akiwasilisha Kero hiyo, Mwenyekiti Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Longido Joseph Laizer, ameishukuru Serikali na kuipongeza kwa miradi mingi inayoteklezwa kwenye Tarafa hiyo ya Ketumbeine, husasni ujenzi wa Kituo cha Afya, kituo ambacho amaekiri ni cha kisasa na kinatoa huduma nzuri kwa wananchi hao.
Aidha, ameeleza changamoto kubwa ya afya inayowakabili wanachi hao, ni ukosefu wa chumba cha kuhifadhia maiti, na kumuomba mkuu huyo wa mkoa kuona namna ya kujenga chumba hicho kwenye kituo chao cha Afya.
"Mhe. Mkuu wa mkoa, wanachi wa Ketumbeine, tunatambua na kuthamini kazi kubwa iliyofanywa na Serikali yetu ya awamu ya sita chini ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani, ombi letu kubwa, ni kupata chumba cha mochuari kwenye kituo cha afya Ketumbeine, tunatumia gharama kuwa pindi watu wanapofariki kwenda mbali kuhifadhi miili, tunaomba tupate msaada huo, ili huduma hii ipatikane kwenye hospitali yetu" Ametoa ombi hilo mwenyekiti huyo mstaafu.
Awali mkuu wa mkoa wa Arusha, amepokea kero za wananchi hao na kuziagiza Mamlaka husika kuzitatua ndani ya kipindi cha mwezi mmoja mpaka mitatu.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.