Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mhe. John V.K Mongella, ameshiriki hafla ya kufunga Mafunzo ya Teknolojia ya 3D Printing shule ya Sekondari Arusha Sayansi, ambapo jumla ya wanafunzi 53 wamehitimu mafunzo.
Mhe. Mongella, licha ya kuupongeza uongozi wa shule hiyo, kwa kuandaa mafunzo hayo, amekiri kushuhudia mazingira bora yenye miundombinu ya kiteknolojia ikiwemo maabara za kisasa zilizopo shuleni hapo.
"Serikali ya awamu ya sita inaendelea kuweka mazingira rafiki kwenye sekta ya elimu na hii ni ishara tosha ya namna ambavyo Shule, inaawaandaa vyema wanafunzi na kuwapa ujuzi wa kiteknolojia wanafunzi hawa kwenye maisha yao na taifa letu la Tanzania.
Aidha, amewataka kuendelea kutoa mafunzo hayo ili yaweze kuwanufaisha wanafunzi wengine zaidi, kwa kuwa dunia ya sasa, inaendeshwa kiteknolojia, mafunzo hayo yanawaandaa vijana kuweza kuingia kwenye ushindani wa soko la ajira ndani na nje ya nchi
Naye Mmliki wa Shule hiyo Prof. Juma Hatibu, amesema kuwa Serikali inayo Sera nzuri ya elimu ambayo inachochea uzalishaji wa vijana wenye maarifa ya kisayansi, ambayo ina uwezo wa kutatua matatizo ya kijamii nchini.
Aidha, amebainisha kuwa 3D Printer, ni teknolojia yenye uwezo wa kuchapisha picha kwa teknolojia ya kisasa yenye uwezo wa kuchapisha picha kwa pande zote.
Hata hivyo wahitimu hao, wamepongeza na kushukuru uwepo wa teknolojia hiyo, utakaowawesha kujifunza kwa wepesi kwa kutengeneza zana za kujifunzia wenyewe.
Rose Nehemia, mhitimu wa mafunzo hayo, amesema mashine ya 3D Printing ni teknolojia mpya nchini, ambayo itarahisisha na kusaidia kutengeneza vitu vingi ambavyo vitawasaidia katika masomo yao ikiwemo zana za kujifunzia.
Mafunzo hayo yaliandaliwa na shule hiyo kwa kushirikiana na wadau, ambao ni watanzania waishio Marekani, ambayo amekiri ni ishara njema kwa uongozi wa Shule unavyopambana kuhakikisha wanafunzi wanakuwa bora.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.