Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. John V.K Mongella, ameipongeza Sekretarieti ya Mkoa huo, kwa kushirikiana katika kufanya kazi na kila mmoja kutimiza wajibu na majukumu yake, weledi ambao umesababisha Mkoa huo kuwa na matokeo chanya na kufikia malengo ya kiutumishi kwa mwaka 2023.
Mhe Mongella ameyasema hayo, wakati wa sherehe za kukaribisha mwaka mpya 2024, zilizowakutanisha watumishi wa Mkoa huo, pamoja ja Taasisi , mashirika ya Umma na ya binafsi, zilizofanyika kwenye, Kituo cha Mikutano ya Kitaifa (AICC), Ukumbi wa Nyasa, Jijini Arusha.
Ameweka wazi kuwa, kasi ya Maendeleo inayofanywa na Serikali ya awamu ya sita katika sekta zote, inachagizwa na watumishi wa Mkoa wa Arusha, kwa umoja na ushirikiano kwa kila mmoja kutimiza wajibu na majukumu aliyokasimiwa na Serikali kulingana na taaluma yake.
"Ninafurahishwa na kazi kubwa inayofanywa na watalaam wa sekta zote, kwa kushirikiana na Taasisi na mashirika ya Umma na ya binafsi na kuhakikisha fedha za miradi ya Maendeleo, zinazoletwa kwenye Mkoa wetu zinasimamiwa vizuri na utekelezaji wake na kufikia malengo ya Serikali licha ya changamoto zilizopo"
Aidha amempongeza Katibu Tawala Mkoa huo, Missaile Albano Musa kwa kazi nzuri anayoifanya ya kuwaunganisha watumishi wote wa Mkoa wa Arusha pamoja.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.