*MAKABIDHIANO YA HATI*
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mhe. John V.K Mongella, amemkabidhi Hati Miliki ya eneo lenye ukubwa wa Ekari 39, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Damas Damian Ndumbaro, leo tarehe 18 Desemba, 2023.
Mhe. Mongella amekabidhi Hati Miliki ya eneo lililopo Mtaa wa Murongoine, kata ya Olmoth, Jiji la Arusha, kwa ajili ya kujenga uwanja wa mpira wa miguu,ikiwa ni maandalizi ya mashindano ya AFCON yanayotarajiwa kufanyika mkoani Arusha mwaka 2027.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.